IGUNGA WORRIERS YAUA KAMA KAWAIDA YAO BILA HURUMA..GOLI 7-0


Jana  mapema  uwanja  wa saba saba  wilayani  IGUNGA mkoa  wa TABORA  kulipigwa  mchezo  mkali  wa  kukata  na  shoka, chama  linalosumbua  wilayani IGUNGA  WORRIERS  walimenyana  vikali  na  vijana  wa  MAKOMERO FC pambano  lilioshuhudiwa  wa  washabiki  lukuki  kana  kwamba  timu  zote  zilikuwa  vizuri  kwa  kuzingtia timu  ya  MOKOMERO ilikuwa  na  wachezaji  wa  ndondo ambao  alifanya  mechi  kuwa  yenye  mvuto  na  kuvutia  wadau  wengi  wa  soka .

 Japo mechi  ilitazamiwa  kuwa  na  ushindani  lakini ilionekana  kuwa  rahisi  xana  kwa   upande  wa  mashujaa  wa igunga (IGUNGA  WORRIERS) baada  ya  kuwashushia  kipigo  kikali  wapinzani   wao mabao 7-0,  mabao  yaliyofungwa  na MSWETI, MESS, SAIMON   SHILE a.k.a ZOLA naye mshambuliaji  mahiri  wa  anayelijua goli SALUMU BENSO  BAJA ligunga magoli manne(4) katika  mchezo  wakati  huo   huo wamekosa  magoli  mengi wa  wazi  na  kubaniwa  baadhi  ya  penalt  zahiri.

Akizungumza kocha  IGUNGA WORRIERS  bwana CHISANO  amedai  kulifanyia  kazi  suala  la  umaliziaji kwani  ndilo  limekua tatizo  sugu katika  timu  yake  kwani  idara  zote  timu  iko  vizuri    naye kocha  wa  MAKOMERO FC ameahidi  kujipanga  vizuri  ili  kufanya  vizuri  mechi  ya  mwisho iliyobaki dhidi  ya MWANA AFRICA.

Ikiwa  ni  hatua  ya  makundi  katika  kikombe  cha EID L HADJI CUP  leo  jioni  mapema  ATOMIC BOMU wataumana na  vijana  toka  stoo  yaani  STOO  FC
IGUNGA WORRIERS YAUA KAMA KAWAIDA YAO BILA HURUMA..GOLI 7-0 IGUNGA  WORRIERS  YAUA KAMA  KAWAIDA  YAO  BILA  HURUMA..GOLI  7-0 Reviewed by Unknown on 7:10:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.